Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) imeendelea na ujenzi wa miundombinu ya umeme kwa kutumia wataalamu wazawa katika utekeleza mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 132 kutoka Mkoa wa Tabora hadi Katavi.
