ETDCO imekamilisha ujenzi wa Mradi wa REA III, Mzunguko wa Pili, Mkoani Mbeya. Mradi huo umewezesha zaidi ya wateja 7,546 na vijiji 152 kunufaika na huduma ya umeme.
Ujenzi huo umehusisha njia ya kusafirisha umeme ya kilovolti 33 yenye urefu wa kilomita 500, na njia ya kusambaza umeme ya kilovolti 0.4 yenye urefu wa kilomita 429.
